Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya Bambuti yategemea kurejeshwa kwa uhifadhi wa Okapi DRC

Jamii ya Bambuti yategemea kurejeshwa kwa uhifadhi wa Okapi DRC

Msitu wa Epulu ambao umeorodheshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni UNESCO kama urithi wa dunia umesheheni bayoanuai.

Miongoni mwa maajabu yanayopatikana kwenye msitu huu pekee duniani kote ni aina ya mnyama adimu sana, aitwaye Okapi.

Msitu huo pia ni makazi ya jamii ya watu wa asili wa Pygmee wanaofahamika kama Bambuti, ambao maisha yao yalikuwa yanategemea wanyama pori. Lakini maisha hayo sasa yako hatarini.

Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hiyo iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Idara ya Mawasiliano ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO.