Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulinzi wa mambo ya kale ni suala la kimataifa:UNESCO

Ulinzi wa mambo ya kale ni suala la kimataifa:UNESCO

Ulinzi wa kazi za kihistoria za Sanaa sio tu suala la wakati wa migogoro au vita bali ni suala linalotia hofu kimataifa limesema shirika la Umoja wa mataifa la Elimu , Sayansi na Utamaduni UNESCO.

Huo pia ni mtazamo wa Dr Donna Yates mhadhiri wa usafirishaji haramu wa mambo ya kale na uhalifu wa Sanaa katika chuo kikuu cha Glasgow nchini Scotland.

Dr Yates anashiriki majadiliano kuhusu usafirishaji wa mali za kitamaduni yaliyoandaliwa na UNESCO mjini Paris leo Jumatano. Anaelezea ni maeneo gani hasa yaliyo katika hatari ya kuporwa.

(SAUTI YA DR YATES 1)

"Endapo nitasema Iraq, Syria au Libya au Yemen ntakuwa nimepuuza tutakuwa tunapuuza hizo sehemu zingine , kwa kweli ni suala la kimataifa, sio suala la sehemu moja tu ."

na nini kifanyike kuhusu hali hii

(DR YATES

“Nitapenda kuwe na mjadala mkali wa wazi na miongoni mwa wadau kuhusu wigo wa takwimu gani wanazuoni na serikali zinaweza kuziwasilisha kuhusu uporaji wa mali za kitamaduni”