Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asiachwe mtu nyuma, tutimize lengo la afya kwa wote- WHO

Asiachwe mtu nyuma, tutimize lengo la afya kwa wote- WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO), limetowa wito wa kutomwacha mtu yeyote nyuma katika kutimiza lengo la kuwezesha huduma ya afya kwa wote. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(Taarifa ya Joshua)

Ujumbe huo umetolewa na WHO kanda ya Kusini Mashariki mwa Asia, ambako watu wapatao milioni 130 katika kanda hiyo hawapati huduma muhimu za afya, huku wengine milioni 50 wakishinikizwa kuwa maskini kutokana na gharama za matibabu.

WHO imesema nchi katika kanda hiyo zinapaswa kuchukua hatua za dharura na madhubuti, ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, na kuendeleza afya ya watu wote.

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Kusini Mashariki mwa Asia, Dkt. Poonam Khetrapal Singh, amesema huduma ya afya kwa wote inamaanisha kuwa watu wote wanaweza kupata huduma za afya wanazohitaji bila kukumbana na matatizo ya kifedha, wawe tajiri au maskini, na bila kujali wanapoishi.