Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajumbe wa Quartet wakutana wa wakilishi wa Israel na Palestina

Wajumbe wa Quartet wakutana wa wakilishi wa Israel na Palestina

Mapema wiki hii wajumbe wa mkutano wa pande nne kwa ajili ya Mashariki ya Kati Quartet wamekutana mjini Jerusalem na kufanya majadiliano na upande wa Israel na Palestina.

Wajumbe hao kutoka Urusi, Marekani, Muungano wa Ulaya na Umoja wa mataifa , wamekutana Jumatatu Machi 28 kujadili maandalizi kwa ajili ya ripoti ya Mashariki ya Kati ya Quartet itakayotolewa hivi karibuni.

Wakati wa ziara yao pia wametumia fursa hiyo kukutana na maafisa kutoka ofisi ya waziri mkuu wa Israel na wizara ya mambo ya nje pamoja na maafisa kutoka chama cha Palestine Liberation Organization (PLO) na mamlaka ya Palestina.