Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuwapa makazi asilimia 10 ya wakimbizi milioni 4.8 wa Syria ifikapo 2018:IOM

UM kuwapa makazi asilimia 10 ya wakimbizi milioni 4.8 wa Syria ifikapo 2018:IOM

Umoja wa Mataifa una lenga kuwapa makazi zaidi ya wakimbizi 450,000 wa Syria ifikapo mwaka 2018, ikiwa ni takribani moja ya kumi ya wakimbizi wote ambao sasa wako katika nchi jirani.

Lakini shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linakubali kwamba linahitaji kukabili hofu iliyotanda limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

UNHCR imezitaka nchi zote duniani kuwachukua Wasyria na kuwapa makazi lakini pia kwa sababu za kibinadamu kuweza kuwaunganisha na familia zao, kuwapa huduma za afya au ufadhili wa shule kuweza kuhimisha masomo yao.

Zaidi ya wakimbizi milioni 4.8 wa Syruia wamekimbilia Uturuki, Lebanon, Jordan na Misri wakikimbia vita ambavyo tayari vimeshakatili maisha ya watu Zaidi ya 250,000, tangu vilipozuka mwaka 2011 na kuwaacha wengine milioni 13.5 ndani ya Syria wakihitaji msaada.