Skip to main content

Ban akaribisha hatua ya AUHIP , Sudan ya kusitisha mapigano

Ban akaribisha hatua ya AUHIP , Sudan ya kusitisha mapigano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha mpango wa karibuni wa jopo la ngazi ya juu la utekelezaji la Umoja wa Afrika (AUHIP) kwa Sudan na Sudan Kusini kuleta pamoja Serikali ya Jamhuri ya Sudan, National Umma Party, Sudan People Liberation Movement / North, Justice and Equality Movement na Sudan Liberation Movement / Minni Minawi kufikia makubaliano juu ya ukomeshaji wa uhasama, upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na mchakato wa mazungumzo ya umoja wa kitaifa .

Amekaribisha pia serikali ya Sudan kutia saini hapo Machi 21 mwaka huu mpango wa makubaliano uliopendekezwa na AUHIP.

Ametoa wito kwa serikali kutekeleza kikamilifu makubaliano na kuzitaka pande zote kutia saini pia mapendekezo hayo. Amesema hii itakuwa hatua muhimu katika kuelekea kukomesha vita , kutoa msaada kwa jamii zinazohitaji na kuboresha mazingira ya mjadala wa kitaifa utakaojumuisha pande zote.