Nasikitishwa kuendelea mapigano Sudan Kusini: Mogae

28 Machi 2016

Mwenyekiti wa kamisheni ya pamoja ya kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini, JMEC Festus Mogae, ameonyesha wasiwasi wake kuhusu uchelewashwaji wa usitishwaji wa mapigano ambao amesema unaendelea kudidimiza uchumi wa taifa hilo change.

Akiongea katika mkutano wa kamisheni hiyo Mogae ambaye pia ni Rais mstaafu wa wa Botwasana amewaambia wajumbe wa JMEC kuwa anapaswa kuripoti kwa baraza la usalama utekelezaji wa makubaliano lakini akasema.

( SAUTI MOGAE)

‘‘Hebu niwe mkweli na niwaambie kwamba uvumilivu wa jumuiya ya kimataifa pamoja nami unapimwa. Nikiendelea kusalia mwenye matumaini kama sote pia, sasa ni wakati wa kuthibitisha kwamba ahadi ambazo zimerudiwa na pande husika ni za kweli .’’

Mikutano ya kamisheni ya kufuatilia tathimini ya makubaliano ya amani hujaidli pia hatua zilizochukuliwa na pande kinzani katika misaada ya kibinadamu na usitishwaji wa mapigano.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter