Mkuu wa UNESCO na Rais Putin wajadili ulinzi wa Palmyra, Syria

28 Machi 2016

Kufuatia kukombolewa kwa mji wa Palmyra nchini Syria, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Irina Bokova, amefanya majadiliano kwa njia ya simu na Rais Vladimir Putin wa Urusi kuhusu kulinda na kuhifadhi urithi wa kitamaduni wa mji huo.

Katika majadiliano hayo, Bi Bokova amesema yuko tayari kutuma ujumbe wa wataalam wa UNESCO wa kutathmini dharura, ili wafanye tathmini ya uharibifu uliofanywa dhidi ya eneo la UNESCO la Urithi wa Dunia, Palmyra mara tu hali ya usalama itakavyowezesha kufanya hivyo.

Rais Putin amemweleza Bi Bokova kuwa yu tayari kutoa usaidizi na utaalam wa nchi yake mara moja kwa ujumbe wa wataalam wa UNESCO, kadri hali ya usalama itakavyowezesha, pamoja na kumhakikishia kuhusu usaidizi katika kuhifadhi na kukarabati eneo la urithi wa kitamaduni la Palmyra.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter