Ban akutana na Rais Abbas wa Palestina

27 Machi 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amekutana na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina, ambapo amekariri masikitiko yake makubwa kuhusu ghasia zinazoendelea sasa, na haja ya pande kinzani kuimaliza hali ya utata.

Ban ambaye yupo ziarani Mashariki ya Kati kupigia debe mkutano kimataifa masuala ya kibinadamu mjini Istanbul, mwezi Mei, amesisitiza haja ya kuendeleza hatua za umoja wa Palestina, nay a uongozi wa dhati katika kuijenga upya Gaza.

Aidha, viopngozi hao wawili wamejadili kuhusu mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati, ukiwemo mchango wa nchi nne.

Ban amekariri kuwa mazingira mapya ya kisiasa yanapaswa kuwekwa hima kwa ajili ya kurejelewa mazungumzo ya amani kuhusu suluhu la mataifa mawili.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter