Ban azungumza kwa simu na Rais Petro Poroshenko wa Ukraine

23 Machi 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na rais wa Ukraine, Petro Poroshenko.

Simu hiyo ilipigwa kwanza na Rais Poroshenko, ambaye amempaazia sauti raia wa Ukraine, Nadiya Savchenko, ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 22 gerezani na mahakama ya mji wa Donestsk, katika eneo la Rostov-on-Don la Urusi.

Katibu Mkuu amemweleza Rais Poroshenko kuwa anafuatilia kwa karibu kesi ya Bi Savchenko, ikiwemo kukiukwa kwa viwango wastani vya kuendesha mashtaka na haki ya mshukiwa katika kesi nzima. Ametilia msisitizo matarajio yake kwa nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa kutimiza viwango wastani vinavyokubaliwa kimataifa vya kuendesha mashtaka na matumizi ya sheria.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter