Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yawasili Taizz na msaada wa kuokoa maisha

UNHCR yawasili Taizz na msaada wa kuokoa maisha

Mapema wiki hii shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR lilituma malori 13 yaliyosheheni msaada yakiwemo mablanketi, magodoro na vitu vingine vya dharura vinavyohitajika kwenye jimbo la Taizz nchini Yemen.Flora Nducha anafafanua

(TAARIFA YA FLORA)

Kwa mujibu wa shirika hilo hii ni hatua ya faraja ikizingatiwa kwamba ni mara ya kwanza msafara wa UNHCR umefanikiwa kuingia hadi Taizz ukitokea Aden. Msafara huo ulitumwa kwa ushirikiano na kamati ya misaada ya serikali ya Yemen na umewasili Jumapili na ugawaji wa misaada unaanza wiki hii kwa wakimbizi wa ndani 500 wengi wao wakiwa waliorejea Taizz lakini pia pamoja na familia za eneo hilo zilizoathirika na vita.

Malori mengine 13 yako njia karibu na jimbo la jirani la Sabri Al Mawadim na msaada huo utagawanywa kwa familia zingine 500. Wilaya hizo mbili zinahifadhi wakimbizi wa ndani 7,500 lakini Taizz pekee ina wakimbizi wa ndani 555,048.