Chombo maalum kifuatilie Sudan Kusini- Simonovic

23 Machi 2016

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Ivan Simonovic amependekeza hatua za kuchukuliwa na Baraza la haki za binadamu ili kuepusha kupuuzwa kwa maisha ya binadamu na ukepwaji sheria unaoendelea Sudan Kusini.

Akihutubia Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi lililokutana kupata ripoti kuhusu Sudan Kusini, Simonovic amesema ni dhahiri kuwa pande kinzani zinakiuka haki za binadamu ikiwemo ubakaji, utumikishaji watoto, na kwamba hata kama kuna maridhiano ni lazima kufuatilia utekelezaji, hivyo akapendekeza Baraza hilo...

(Sauti ya Simonovic)

Lifikirie kuanzishwa kwa chombo maalum, mahsusi kwa ajili ya kuripoti maendeleo kuhusu uwajibikaji na hali ya kibinadamu.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter