Skip to main content

Vyombo vya habari vyahimizwa kukuza usawa wa jinsia

Vyombo vya habari vyahimizwa kukuza usawa wa jinsia

Vyombo vya habari ni vyanzo vya uwezeshaji wa wanawake na usawa wa kijinsia, wamesema leo washikiri wa mjadala maalum uliofanyika sanjari na mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW60.

Washiriki hawa wamehimiza mashirika makubwa ya vyombo vya habari kupazia zaidi sauti za wanawake katika vipindi vyao, wakisisitiza kwamba vyombo vya habari vinaweza kuchangia pakubwa katika kuelimisha jamii kuhusu masuala yanayohusiana na usawa wa jinsia.

Phumzile Mlambo Ngcuka ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women.

( Sauti ya Phumzile)

“Tunahitaji wanawake zaidi kwenye majukumu ambayo yanaonekana kwenye vyombo vya habari na ambao wanaweza kuongea na kusema vitu vya maana. Si mstari mmoja tu au “ha ha ha”. Ukiwa nyota na kuimba mbele, wale walio nyuma wanafanya “ooz”na “aaz”, wanawake hawataki kufanya ooz na aaz, wanataka kuwa kwenye mstari wa mbele na kusema vitu vya maana zaidi.”

Bi Mlambo Ngcuka amesisitiza pia kwamba wanawake wanapaswa kupewa nafasi zaidi kwenye uongozi wa vyombo vya habari.