Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukraine: lazima kuwe na uwajibikaji wa ukiukwaji wa haki za binadamu

Ukraine: lazima kuwe na uwajibikaji wa ukiukwaji wa haki za binadamu

Kikosi kazi cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya askari mamluki kimetoa wito kwa serikali ya Ukraine kuhakikisha uwajibikaji kwa ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa na wageni wenye silaha wakati wa machafuko yaliyoikumba nchi hiyo tangu mwaka 2014.

Wageni hao wenye silaha ni kuanzia watu wa kujitolea hadi wafanyakazi wa kike na kiume na pia makundi huru ya wanamgambo hadi wanajeshi. Ujumbe wa kikosi kazi hicho unaoundwa na watalaamu wa haki za binadamu Patricia Arias na Saeed Mokbil, wameelezea hofu yao kuhusu madai ya mamluki kujiunga na pande zote za mgogoro wa Ukraine jambo ambalo wamesisitiza linapingwa vikali chini ya sharia za kimataifa.

Katika mwisho wa ziara yao ya siku tano nchini Ukraine wataalamu hao wamebainisha kwamba ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo umearifiwa kutendwa sio tuu na mamluki lakini pia wapiganaji wa kigeni.

TWataalamu hao wamearifiwa na uongozi wa Ukraine kwamba kuna wapigajnaji 176 wa kigeni wanaofanya kazi na makundi yenye silaha katika jimbo la Donetsk na Luhansk. Wapiganaji hao wanajumuisha watu kutoka Urusi, Serbia, Belarus, Ufaransa na Italia miongoni mwao na wanawake pia wamearifiwa kuwepo.

Kikosi kazi hicho kitawasilisha ripoti yake kwenye baraza la haki za binadamu Septemba mwaka huu wa 2016.