Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka mmoja tangu kuzuka machafuko Yemen mfumo wa afya unasambaratika:WHO

Mwaka mmoja tangu kuzuka machafuko Yemen mfumo wa afya unasambaratika:WHO

Mwaka mmoja wa machafuko nchini Yemen umesababisha kuzorota kwa hali ya kibinadamu na mfumo wa afya unasambaratika limesema shirika la afya duniani WHO.

Tangu 19 Machi 2015 hadi 15 Machi 2016, machafuko hayo yamekatili maisha ya watu 6,408 na kujeruhi wengine 30,193 kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo la afya.

WHO inasema sekta ya afya imeathirika vibaya huku asilimia 25 ya vituo vyote vya afya vimefungwa na ambavyo vinafanya kazi vinaghubikwa na madhila mengi ikiwemo hofu ya usalama. Fursa ya dawa za magonjwa sugu kama kisukari, ugonjwa wa moyo na pressure ni finyu .