Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Simonovic ataja mambo muhimu kuleta utangamano Burundi

Simonovic ataja mambo muhimu kuleta utangamano Burundi

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limekuwana kikao kuhusu hali ya kibinadamu nchini Burundi ambapo wajumbe wameelezwa kuwa mwelekeo wa sasa unatia wasiwasi na kwamba mazingira ya mijadala jumuishi ya pande zote yanatakiwa ili kuondoa mgawanyiko na msambaritiko wa jamii nchini humo. Amina Hassan na ripoti kamili.

(Taarifa ya Amina)

Akihutubia Baraza hilo Ivan Simonovic, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu amesema mgawanyiko nchini humo umetokana na umaskini na mvutano wa kisiasa na hivyo kinachotakiwa ni hakikisho la uhuru wa kujieleza, vyombo vya habari kuwa huru na pia.

(Sauti ya Simonovic)

“Lazima kutokomeza tabia ya watu kupotea, kukamatwa kiholela au mauaji na utesaji kinyume cha sheria,na hatua za wazi za kisheria kwa umma kuwajibisha watekelezaji wa uhalifu wakiwemo mawakala wa serikali na wanajeshi.”

Kwa upande wake Pierre Claver Mbonimpa, Rais wa chama cha ulinzi wa haki za binadamu wanaoshikiliwa, APRODH akahoji Baraza..

(Sauti ya Mbonimpa)

“Mko hapa kwa ajili ya haki za binadamu, je haki za binadamu hazikukiukwa Burundi? Sasa mtafanya nini? Hicho ndio ndio tunasubiri.”

Mapema Bwana Simonovic alieleza kuwa tangu kuanza kwa mzozo mwaka jana zaidi ya watu 4951 walikamatwa ambapo hata hivyo hadi sasa 3117 wameachiliwa huru ilhali 1834 bado wanashikiliwa.