Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Liberia kukabidhi elimu ya msingi na chekechea kwa kampuni binafsi haikubaliki- UM

Liberia kukabidhi elimu ya msingi na chekechea kwa kampuni binafsi haikubaliki- UM

Ni suala lisilokubalika kabisa kwa Liberia kukabidhi mfumo wa elimu yake ya msingi kwa kampuni binafsi , amesema mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya elimu Kishore Singh. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Taarifa ya Joshua)

Amesisitiza kuwa mapendekezo hayo hayakubaliki kwa kiwango kikubwa na yanakiuka majukumu ya kisheria na kimaadili ya Liberia. Mpango wa Liberia ni kubinafsisha shule zote za msingi na chekechea kwa miaka mitano ijayo. Ufadhili wa umma utasaidia huduma ambazo zitaendeshwa na kampuni binafsi ijulikanayo kama -the Bridge International Academies.

Amesema kwa mantiki hiyo shule za umma na waalimu wao na dhana ya elimu bora ya umma vitakuwa matatani, jambo ambalo Liberia itakuwa imekiuka wajibu wake wa kimataifa wa haki ya elimu na haina sababu ya msingi ya kufanya hivyo chini ya katiba yake.

Ameongeza kuwa hili pia linaenda kinyume na ahadi za kisiasa zilizotolewa na Liberia kwa kujumiya ya kimataifa kwenye kwenye mkutano wa nne wa maendeleo endelevu.

Bwana Singh ameitolea wito serikali ya Liberia kuwasiliana na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO kwa msaada wa kiufundi na uwezeshaji badala ya kuingia ubia na kampuni binafsi.