Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvutano wa kisiasa unaoighubika Brazil unatia hofu:UM

Mvutano wa kisiasa unaoighubika Brazil unatia hofu:UM

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa hofu na ongezeko la mvutano wa kisiasa na mjadala ulioighubika Brazili katika wiki chache zilizopita.

Imeitaka serikali na  wanasiasa kutoka vyama vyote kutoa ushirikiano kikamilifu kwa mfumo wa sharia nchini humo katika uchunguzi wake wa madai ya ufisadi wa hali ya juu na kuepuka hatua zozote ambazo zitaingilia au kuwa kikwazi cha kupatikana kwa haki.

Wakati huo huo wameutaka uongozi wa mfumo wa sheria kutekeleza wajibu wake kwa misingi ya sheria za kitaifa na kimataifa na kuepuka kuelemea mitazamo ya kisiasa.