Ban akaribisha hukumu ya ICC dhidi ya Jean-Pierre Bemba:

22 Machi 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha hukumu iliyotolewa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC Jumatatu dhidi ya kesi ya Jean-Pierre Bemba raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jean-Pierre Bemba alikuwa kamanda wa kundi la waasi wa Congo la Movement for the Liberation of Congo (MLC), na pia makamu wa Rais wan chi wakati wa kipindi cha mpito mwaka 2003 hadi 2006.

Bwana Bemba amekutwa na hatia ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa vita ikiwemo ubakaji, mauji na uporaji vilivyotekelezwa kati yam waka 2002 na 2003 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Ban amesema hukumu hiyo ya mahakama inadhihirisha kwamba ukwepaji wa sharia hautovumiliwa na ni ishara kwamba makanda watawajibishwa kwa uhalifu wa kimataifa unaofanywa na walio chini ya mamlaka yao.

Ban anatambua kuwa hukumu hiyo ni hatua muhimu ya kuwapa haki waathirika kwa ukatili na uhalifu mkubwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na kusistiza umuhimu wa kushughulikia ukwepaji sharia kwa nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati na DR Congo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter