Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa wito kwa mataifa na wadau kuungana kutokomeza TB

WHO yatoa wito kwa mataifa na wadau kuungana kutokomeza TB

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya kifgua kikuu (TB) duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 24, shirika la afya ulimwenguni WHO limetoa wito kwa nchi na washirika kuungana kutokomeza kifua kikuu.

Wito huo umekuja wakati tunaingia katika utelkelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s. Na kutokomeza kifua kikuu ifikapo 2030 ni lengo la SDG’s na pia pia lengo la mkakati wa WHO kutokomeza TB.

Kwa mujibu wa WHO wakati kuna hatua kubwa imepigwa katika vita dhidi ya kifua kikuu ambapo maisha ya watu milioni 43 yameokolewa tangu mwaka 2000, vita vimefaulu kwa nuisu tuu, huku watu zaidi ya 4000 wakipoteza maisha kila siku kutokana na ugonjwa huo wa kuambukiza.

Shirika hilo linasema nchi nyingi zinazolemewe na mzigo wa TB ni zile jamii masikini, zisizojiweza na zilizotengwa. Limesema mafanikio ya kutokomeza TB yatafikiwa tuu kwa ushirikiano mkubwa ndani na miongoni mwa serikali zote ikiwa ni pamoja na washirika kutoka jumuiya za kiraia, jamii, watafiti, sekta binafsi na mashirika ya maendeleo.