Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni lazima serikali washirikiane na watetezi wa haki za bindamu hususan wanawake-Bi.Ali

Ni lazima serikali washirikiane na watetezi wa haki za bindamu hususan wanawake-Bi.Ali

Wakati mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake umeingia wiki ya pili, vikao mbali mbali vimefanyika, mada mbali mbali zikijadiliwa ikiwemo haki za wanawake na watoto wa kike. Katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa Idhaa hii Bi Saida Ali mwanaharakati kutoka Kenya anayewakilisha Mashirika mawili Raising voices na FEMNET amesema kwamba ni muhimu kwamba serikali na watetezi wa haki za bindamu wakafanya kazi pamoja ili kufanikisha jamii badala ya wao kuonekana kama wapinzani wa serikali, na hapa anaanza kwa kuelezea shughuli zao.