Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya Down Syndrome , ujumuishwaji wasisitizwa

Siku ya kimataifa ya Down Syndrome , ujumuishwaji wasisitizwa

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Ugonjwa unaoathiri uwezo wa kujifunza au Down Syndrome maudhui ya mwaka huu yanaeleza faida za ujumuishwaji kwa ajili ya watoto ambao ni watu wazima wa kesho. Priscilla Lecomte na maelezo kamili.

( TAARIFA YA PRISCILLA)

Ujumbe wa mwaka huu unasisitiza kuwajumuisha watoto wanaozaliwa na ugonjwa huo, ambapo kuwathamini kama sehemu ya jamii kunatiliwa mkazo.

Katika mahojiano na idhaa hii Mkurugenzi wa taasisi ya Uganda ya watoto wanaozaliwa wakiwa na kasi ndogo ya kujifunza Dk Okiro Obwokor anasema kile ambacho jamii hususani ya Afrika inapaswa kufanya ili kuwawezesha watoto wenye ugonjwa huo.

( SAUTI DK OKIRO)

Na je watoto wanaozaliwa katika hali hiyo wana uwezo gani?

( SAUTI DK OKIRO)