Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laangazia jinsi ya kudumisha amani kwenye ukanda wa Maziwa Makuu

Baraza la Usalama laangazia jinsi ya kudumisha amani kwenye ukanda wa Maziwa Makuu

Leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala maalum kuhusu kuzuia na kutatua mizozo kwenye ukanda wa Maziwa Makuu, Katibu Mkuu Ban ki-moon akimulika changamoto zinazoendelea kuhatarisha usalama wa ukanda huo. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Bwana Ban amesema kwamba licha ya mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa Ujumbe wa Umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC miaka 16 iliyopita hasa kwa upande wa utawala wa demokrasia, ukosefu wa usalama na mivutano ya kikabila mashariki mwa nchi na kwenye nchi jirani ya Burundi vinatia wasiwasi.

Amewaomba viongozi wa ukanda huo kushirikiana ili kuhakikisha vikosi hasimu vinajisalimisha, hasa FDLR na ADF, akisisitiza pia umuhimu wa kudhibiti biashara haramu ya mali asili ambayo hufadhili mizozo.

Kuhusu mwelekeo wa uchaguzi nchini DRC akaongeza:

(Sauti ya Ban)