UNESCO yalaani vikali mauaji ya mtangazaji wa Radio João Valdecir de Borba nchini Brazil

21 Machi 2016

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO), Bi Irina Bokova, leo ameitaka serikali ya Brazil kuchunguza mauaji ya João Valdecir de Borba yaliyotokea Machi 10 mjini São Jorge do Oeste, kwenye jimbo la Kusini la Paraná, Brazil.

Bi, Bokova amesema analaani vikali mauaji ya mtangazaji huyo wa Radio João Valdecir de Borba na kuongeza kuwa anaamini itawajibika kuchunguza na kuwafiikisha kwenye mkono wa sheria wahusika.

Amesema mauaji haya ya makusudi dhidi ya mwaandishi wa habari aliyekuwa akitimiza wajibu wake , yanaathiri wafanyakazi wote wa vyombo vya habari na uwezo wao wa kutekeleza majukumu yao muhimu ipasavyo.

Watu wawili wasiojulikana walimpiga risasi João Valdecir de Borba alipokuwa akitangaza moja kwa moja kipindi cha muziki kwenye Radio Difusora AM.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter