Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wapaza sauti katika Mkutano wa sitini wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW60

Wanawake wapaza sauti katika Mkutano wa sitini wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW60

Wiki hii hapa kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa pazia la uzinduzi wa mkutano wa 60  kamisheni ya hali ya wanawake limefunguliwa ambapo wanawake wawakilishi wa taasisi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanajumuika kupazia sauti maswala ya kusongesha mbele kundi hilo.

Kauli mbiu ya CSW60 ni uwezeshaji wa wanawake na nafasi yake katika kutimizia malengo ya maendeleo endelevu SDGS sanjari na utokomezwaji wa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ukiangaziwa.

Akifungua pazia hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema hata kama haki ya mwanamke mmoja itakiukwa harakati za ukombozi dhidi yao zitaendelea. Jambo hilo na mengine yametusukuma kusaka wawakilishi kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kufahamu hali ya mwanamke ikoje na ikiwa kuna nuru ya ukombozi.