Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wakiwezeshwa na kuendelea, na nchi inaendelea- Josee Ntabahungu

Wanawake wakiwezeshwa na kuendelea, na nchi inaendelea- Josee Ntabahungu

Wiki ya kwanza ya kikao cha 60 cha Kamisheni kuhusu hali ya Wanawake (CSW60) imehitimishwa hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York Marekani, kikao hicho kikiwa kimewaleta pamoja wanawake na wanaharakati wa haki za wanawake kutoka kote duniani.

Mmoja wa washiriki kutoka Afrika Mashariki, ni Josee Ntabahungu, Meneja wa Programu ya Kuendeleza Wanawake katika Shirika la Care International, nchini Burundi.

Akihutubia kikao cha jopo la ngazi ya juu cha CSW60 wiki hii, alihimiza haja ya ushirikiano katika uratibu na uwekezaji katika miradi ya wanawake ili kuwawezesha wanawake kifedha.

Baadaye, Joshua Mmali alimuuliza kwa nini anapazia sauti uwekezaji katika wanawake

(Mahojiano na Josee Ntabahungu)