Sasa tusema hapana #Ukeketaji watoto wa kike - Kakenya Ntaiya

Sasa tusema hapana #Ukeketaji watoto wa kike - Kakenya Ntaiya

Mila potofu au mila zilizopitwa na wakati, ni moja ya ajenda zilipatiwa kipaumbele katika mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW60 unaoendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hadi tarehe 24 mwezi Machi mwaka huu. Tamaduni kama vile ukeketaji watoto wa kike na wanaume, vipigo vya majumbani ni miongoni tu kati ya mambo mengi yanayokumba wanawake na watoto wa kike na hivyo kukandamiza haki zao na kuwarudisha nyuma kila uchao. Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA linapigia chepuo harakati za kutokomeza mila na vitendo hivyo na katika mkutano huu UNFPA haikuwa nyuma kwani imeandaa tukio maalum kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii.