Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa usawa wa kijinsia kwenye vyombo vya habari waangaziwa

Ukosefu wa usawa wa kijinsia kwenye vyombo vya habari waangaziwa

Changamoto katika usawa wa kijinsia kwenye vyombo vya habari leo umeangaziwa wakati wa mijadala ya mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW60 unaoendelea jijini New York. Priscilla Lecomte na taarifa kamili.

( TAARIFA YA PRSCILLA)

Mjadala huo umeandaliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ambapo wadau wa masuala ya jinsia na habari wameelezea umuhimu wa usawa wa jinsia katika upashanaji wa taarifa.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema shirika hilo limeunda muungano wa kimataifa wa vyombo vya habari ambao pia unapigia chepuo usawa wa kijinsia na upatikanaji wa taarifa.

Amesema kupitia muungano huo UNESCO imefanya juhudi kuhakikisha ajenda ya usawa wa kijinsia inatekelezwa na kwamba kuna mambo matano muhimu ambayo ni mosi  kuwezesha usawa, pili kuwa na sera madhubuti za kijamii na mikakati, tatu kuelimisha jamii na.

(SAUTI BOKOVA)

‘‘Nne kupitia ubia katika ngazi zote, na tano kupitia utafiti na ufuatiliaji. Nadhani hii ni muhimu sana.’’