Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali mpya ya Myanmar ishughulikie changamoto sugu za haki za binadamu- Mtaalam wa UM

Serikali mpya ya Myanmar ishughulikie changamoto sugu za haki za binadamu- Mtaalam wa UM

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Matifa kuhusu hali ya Haki za Biandamu nchini Myanmar, Yanghee Lee, ameitaka serikali mpya ya Myanmar kushughulikia, changamoto za haki za binadamu zilizokita mizizi katika nchi hiyo.

Akitoa ripoti yake ya pili kwa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, Bi. Lee, ameitolea wito serikali inayoingia madarakani Myanmar, kutumia idhini ya mamlaka iliopewa na wananchi, kukabiliana na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini humo.

Aidha, Mtaalamu huyo ametambua kuwa huenda ikawa vigumu kutokana na mapengo uongozini ambapo ametoa mfano wa asilimia 25 ya viti bungeni ambavyo vimehifadhiwa kwa maafisa wa kijeshi, kinachoweza kuzuia upinzani dhidi ya mabadiliko ya kikatiba.

Bi. Lee, amemtaka Thein Sein, Rais anayeondoka, kutumia majuma yake mawili ofisini kuachilia huru bila masharti, wafungwa wote wa kisiasa wakiwemo wanafunzi, wanaharakati wa ardhi na watetezi wa haki za binadamu na kutupilia mbali mashtaka dhidi yao.

Ameonya kuwa, watu wataendelea kufungwa kisiasa mpaka pale sheria inayokandamiza wakosoaji wa serikali itakapofutwa.