Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji safi na salama ni msingi kwa mabilioni ya wafanyakazi duniani: ILO

Maji safi na salama ni msingi kwa mabilioni ya wafanyakazi duniani: ILO

Kila mwaka, wafanyakazi 340,000 hufa kwa sababu ya ukosefu wa maji safi na salama.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kazi Duniani ILO amesema hayo kwenye ujumbe wake wa video kwa ajili ya siku ya maji duniani itakayoadhimishwa tarehe 22 Machi, kwa kumulika uhusiano kati ya maji na ajira.

Ameongeza kwamba watu wapatao bilioni 1.5 wanafanya kazi kuhusiana na sekta ya maji, lakini mara nyingi kazi zao hazitambuliwi wala haki zao za msingi hazilindwi.

(Sauti ya Guy Rider)

“ Chukua mfano wa mwanamke nchini Gambia ambaye anapaswa kutembea saa nyingi kila siku kuchota maji kwa ajili ya familia yake. Hiyo ni kazi. Lakini hailipwi wala haitambuliwi. Iwapo huduma ya maji ingepatikana kwa uhakika, mwanamke huyo angeweza kujifunza stadi ambazo zingemsaidia kupata kazi bora.”