Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siasa na demokrasia wakati mwingine huchagiza ubaguzi:UM

Siasa na demokrasia wakati mwingine huchagiza ubaguzi:UM

Baraza la haki za binadamu leo limekuwa na mjadala kuhusu uwiano baina ya demokrasia na ubaguzi ukitoa fursa ya kutambua changamoto na mbinu bora, kwa lengo la kujikita kuanzia katika changamoto hadi kwa maadili ya kidemokrasia

Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

Akizungumza katika mjadala huo naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu Kate Gilmore ameonya kuanza tena kwa harakati za kibaguzi, za udini, utaifa au chuki za kikabila kwa kutumia jukwaa la siasa.

Amesema nchi zinapaswa kutumia fursa zote, ikiwa ni pamoja kwenye mtandao, ili kukabiliana na usambazaji wa ubaguzi wa rangi na chuki, na kuhakikisha ufanisi ulinzi wa mahakama na tiba kwa waathirika wa ubaguzi wa rangi. Mutuma Rutere  ni mwakilishi maalumu dhidi ya mifumo yote ya kisasa ya ubaguzi anapendekeza kile kinapaswa kufanywa.

(SAUTI YA MUTUMA RUTERE)