Bahrain yatakiwa kumwachilia mwanamke mtetezi wa amani
Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu hali ya watetezi wa amani Michel Forst, leo ametoa wito kwa serikali ya Bahrain kumwaachilia mara moja mwanamke mtetezi wa amani na mwanaharakati wa mitandao ya kijamii Zainab Al-Khawaja, na kumfutia mashitaka yote kwani alikuwa akitekeleza haki yake ya uhuru wa kujieleza.
Bi. Zainab Al-Khawaja alikamatwa pamoja na mwanae wa miezi 15 mnamo tarehe 14 Machi kutokana na mashitaka yanayomkabili kwa ajili ya kuchana picha ya mfalme wa Bahrain na kumtusi mfanyakazi wa umma.
Kwa mujibu wa mwakilishi huyo Bi Zainab anashikiliwa kwa mtazamo wake wa kuikosoa serikali.