Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujali zaidi usalama bila haki hakusaidii kukabili misimamo mikali- UM

Kujali zaidi usalama bila haki hakusaidii kukabili misimamo mikali- UM

Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Kate Gilmore amesema dunia inahitaji haraka iwezekanavyo mwelekeo mpya katika kukabiliana na misimamo mikali.

Akihutubia Baraza la haki za binadamu mjini Geneva, Uswisi, Bi. Gilmore amesema hatu hiyo ni muhimu kwa kuzingatia kuwa mwelekeo wa kuweka usalama mbele umefanya hali kuwa mbaya zaidi katika miaka ya karibuni.

“Madhara ya hatua thabiti za kudhibiti ugaidi zilizochukuliwa baada ya shambulio la Septemba 2001 nchini Marekani yameongeza wigo wa mvutano baina ya jamii, halikadhalika kutoaminiana na kuchochea mgawanyiko mara nyingi kupitia kauli za chuki kwenye mihadhara.”

Awali katika ujumbe wake kwa njia ya video kwa washiriki wa mkutano huo kuhusu misimamo mikali, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka harakati dhidi ya ugaidi ziepuka mbinu za jumlya ambazo zinakandamiza haki za binadamu.

Akiunga mkono kauli hiyo Bi. Gilmore amesema kutokana an vitisho vya sasa kwa jamii vitokanavyo na misimamo mikali, ni muhimu zaidi zama za sasa kuheshimu uhuru wa kuabudu, imani na maoni ya mtu.