Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sokwe mpweke apata makazi mapya huko DR Congo

Sokwe mpweke apata makazi mapya huko DR Congo

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP limesema sokwe aliyepewa jina la Kimia ambayo maana yake amani kwa Kilingala nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekuwa akiishi kama mnyama wa kufugwa nyumbani ingawa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.   Grace Kaneiya anatuhabarisha zaidi.

 (Taarifa ya Grace)

Sokwe huyo yatima alikutwa kwenye kambi ya jeshi na askari wa wanyamapori wa DR Congo na amesafirishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa  kulinda amani MONUSCO hadi kituo cha hifadhi cha Kivu Kusini.

Sokwe huyo anakadiriwa kuwa na umri wa miaka miwili au mitatu atasalia kwenye karantini hadi atakapoungana na sokwe wengine 64 huko Bukavu.

Shirika la GRASP lenye makao yake Nairobi limeshukuru jeshi la Congo na Umoja wa Mataifa kufanishika usafirishaji wa sokwe huyo hadi kwenye kituo maalumu.

Jukumu la MONUSCO mbali ya kulinda amani pia ni kulinda rasilimali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.