Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtu mmoja kati ya kila watano ni mkimbizi Lebanon

Mtu mmoja kati ya kila watano ni mkimbizi Lebanon

Zaidi ya wakimbizi milioni moja wanaishi nchini Lebanon, wakiwa ni sawa na mtu mmoja kati ya kila watano nchini humo, limesema leo Shirika la Umoja wa Mpango wa Maendeleo UNDP.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, UNDP imeeleza kwamba nchi nzima imeathirika na matokeo ya wimbi hilo la wakimbizi lililosababisha idadi ya watu nchini Lebanon kuongezeka kwa asilimia 20.

UNDP imesema hadi sasa imewafikia watu milioni 1.4 nchini humo na misaada mbalimbali, asilimia 75 miongoni mwao wakiwa ni raia wa Lebanon, wengine wakimbizi.

Lengo ni kupunguza mzigo kwa jamii zinazopokea wakimbizi hao, kupitia msaada kwa serikali za mitaa katika kuimarisha huduma za kijamii, miundombinu na pia kuendesha miradi inayolenga kukuza amani na mshikamano wa jamii.