Oman, Umoja wa Mataifa zaandaa mkutano wa baraza linalorasimu katiba Libya

16 Machi 2016

Ufalme wa Oman na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, wametoa mwaliko kwa wanachama wote wa Barza linalorasimu katiba ya Libya (CDA), kwenye mkutano wa mashauriano hapo kesho, kuhusu masuala muhimu ambayo bado hayajatatuliwa. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Rasimu hiyo ya katiba inatazamiwa kutolewa kabla ya kura itakayoamua hatma yake.

Kwenye mkutano wa mashauriano ujumbe wa Umoja wa Mataifa unasaka kusisitiza kanuni ya umiliki wa kitaifa wa katiba ya Libya, ambapo pia watajadili masuala yaliosalia na kuhakikisha kwamba wamekubaliana kuhusu maoni na nyaraka zinazotazamiwa kutolewa.

Ujumbe huo unaamini kuwa, wanachama wote watashirikiana na kuwajibika kwa kuheshimu ibara 30 ya utoaji wa katiba kwa kurasimu katiba inayowakilisha matakwa ya raia wa Libya.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter