Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IMF yaidhinisha mpango mpya wa dola bilioni 1.5 kwa ufadhili Kenya

IMF yaidhinisha mpango mpya wa dola bilioni 1.5 kwa ufadhili Kenya

Shirika la Fedha Duniani IMF limeidhinisha mpango mpya wa ufadhili usiokuwa wa moja kwa moja kwa Kenya, wenye thamani ya dola bilioni 1.5 kupitia mfumo wa sarafu ya fedha na mikopo.

Lengo la ufadhili huo ni kusaidia uchumi wa Kenya kuimarisha uwezo wake wa kustahamili mizozo ya kiuchumi ya kimataifa na majanga ya hali ya hewa.

Taarifa iliyotolewa na IMF imeeleza kwamba ukuaji wa uchumi nchini Kenya ni imara na mwelekeo ni mzuri, wakati ambapo serikali ya Kenya inaendelea kuleta mabadiliko katika matumizi ya umma, huku benki kuu ikijaribu kudhibiti mfumuko wa bei kwa chini ya asilimia 5 kwa mwaka.

Vitaly Kramarenko ni mkuu wa Ujumbe wa IMF nchini Kenya

(Sauti ya Bwana Kramarenko)

“Wakati huo huo Bodi ya Utendaji imepitisha mpango mpya wa ufadhili wa kipindi cha miezi 24, ili kusaidia mamlaka za serikali kukabiliana na udhaifu wake, kusaidia hifadhi zake za kimataifa na kuimarisha sera za msingi kiuchumi”