Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kubaki Afghanistan nchi ikizidi kukumbwa na changamoto

Umoja wa Mataifa kubaki Afghanistan nchi ikizidi kukumbwa na changamoto

Leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuongeza mamlaka ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) kwa kipindi cha mwaka mmoja, mkuu wa UNAMA Nicholas Hayson akisema nchi hiyo imekumbwa na changamoto nyingi za kisiasa, kiuchumi na kiusalama mwaka uliopita, na zinaendelea mwaka huu.

Akihutubia baraza hilo hii leo mjini New york Marekani, Bwana Haysom amesema kwamba changamoto hizo ni pamoja na mzozo wa kiuchumi, machafuko yanayoendeshwa na vikundi vilivyojihami vya Wataliban na mivutano ya kisiasa.

Kuhusu mzozo wa kiuchumi ameeleza kwamba malaki ya vijana wanaotafuta kazi wanakumbwa na ukosefu wa ajira, na ufisadi kwenye sekta binafsi na ya serikali, hali hiyo ikisababisha ongezeko la uhamiaji na ukosefu wa utulivu wa kijamii.

Amesisitiza kwamba ni lazima mazungumzo ya moja kwa moja yafanyike kati ya Wataliban na serikali ya Afghanistan, ili amani iweze kurejeshwa nchini humo.

Hatimaye akakariri

(Sauti ya Bwana Haysom)

“Waafghani 11,000 wamuawa au kujeruhiwa mwaka uliopita, kwa sababu ya mapigano. Robo yao walikuwa ni watoto. Haitoshi tena kwa pande kinzani za mzozo kutoa taarifa kuhusu umuhimu wa kuzuia mashambulizi dhidi ya raia. Wanapaswa kubadilisha jinsi wanaendesha vita.”