Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake vijijini hawanufaiki na uzalishaji na malezi ya kijamii: FAO

Wanawake vijijini hawanufaiki na uzalishaji na malezi ya kijamii: FAO

Licha ya wanawake kubeba jukumu kubwa katika uchumi na malezi ya familia, kundi hilo halifaidiki kutokana na mchango wake, amesema mkuu wa usawa wa kijinsia na maendeleo vijijini katika shirika la chakula na kilimo FAO ukanda wa Afrika Thacko Ndiaye.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa akiwa anahudhuria mkutano wa 60 wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake CSW 60, Bi Ndiaye amesema wanawake wengi hususani viijini hawapati fursa sawa za kibishara katika sekta ya kilimo na hata kutohusishwa katika kamati za ardhi.

( SAUTI NDIAYE)

‘‘Haki za ardhi kwa wanawake bado ni tatizo. Upataji wa fedha nao ni tatizo kubwa, kwani kuna uhusaino kati ya ardhi na upatikanaji wa mikopo. Kama huna hati ya ardhi ni vigumu zaidi kwako kupata mkopo’’

Amesema kutohusishwa kwa wanawake katika vyombo vya uamuzi katika sekta nyeti kama vile kilimo, hufanya uzalishaji wa wanawake kuwa wa kiwango cha chini.