Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya na harakati ajenda #50-50- Waziri Bi. Kariuki

Kenya na harakati ajenda #50-50- Waziri Bi. Kariuki

Mkutano wa sitini wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake, CSW ukiingia siku ya pili huku ikijikita katika kuweka usawa wa 50 kwa 50 kati ya wanawake na wanaume, Kenya imesema  imedhamiria kuhakikisha kiwango hicho kinafikiwa kupitia mikakati mbali mbali iliyojiwekea.

Waziri wa vijana, jinsia na sekta ya umma Cecily Kariuki nchini Kenya amesema hayo katika mahojiano maalum na Idhaa hii kandoni mwa mkutano huo akieleza kwamba serikali ya Kenya imeanzisha mifuko mbali mbali inayoangazia makundi ya walio wachache wakiwemo wanawake ili kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika biashara na sekta mbalimbali ikiwemo…

(sauti ya Bi. Kariuki)

Kadhalikia ameelezea matarajio yake kutoka CSW60

(Sauti ya Bi. Kariuki)