Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashariki mwa DRC, raia wahofia mashambulizi zaidi

Mashariki mwa DRC, raia wahofia mashambulizi zaidi

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, mashambulizi dhidi ya raia yameongezeka tangu mwanzo wa mwaka huu kwenye eneo la mashariki mwa nchi, hasa katika jimbo la Kivu Kaskazini. Visa vya uporaji, ubakaji na mauaji vinazidi kuripotiwa, huku maelfu ya watu wakikimbia makwao kwa hofu ya mashambulizi mengine.

Kwa ushirikiano na jeshi la kitaifa FARDC, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO unajaribu kuchukua hatua ili kupunguza ghasia. Kumulika hali ilivyo katika eneo hilo, ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii