Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamisheni kuhusu madawa ya kulevya yaanza kikao cha 59

Kamisheni kuhusu madawa ya kulevya yaanza kikao cha 59

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC), Yury Fedotov, amesema kuwa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani (UNGASS 2016) kitatoa kipaumbele kwa watu. Joshua Mmali na ripoti kamili.

(Taarifa ya Joshua)

Bwana Fedotov amesema hayo mwanzoni mwa kikao cha 59 cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu madawa ya kulevya (CND), ambacho kinafanyika jijini Vienna Austria.

Mkuu huyo wa UNODC amesema, pamoja na kuandaa kikao cha Baraza Kuu kuhusu madawa ya kulevya kati ya Aprili 19 na 21, kazi ya kamisheni hiyo ni kuchagiza uelewa wa kina kuhusu tatizo la madawa ya kulevya, na haja ya kuweka watu mbele ya mengine yote.

Amesema kote duniani, watu milioni 27 wanataabika kwa matatizo yatokanayo na matumizi ya madawa, wakiwemo watu milioni 12 wanaotumia madawa ya kudunga kwa sindano. Ameongeza kuwa takriban watu 200,000 hufariki kila mwaka kutokana na kuzidisha dozi au matatizo mengine ya madawa.