CSW60 yafungua pazia New York

CSW60 yafungua pazia New York

Mkutano wa 60 wa kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya wanawake, CSW60 umeanza leo jijini New York Marekani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema harakati za ukombozi wa mwanamke zitaendelea hata kama haki ya mwanamke mmoja itakiukwa. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Akihutubia wajumbe kutoka nchi wanachama wa Umoja huo wakiwemo wawakilishi wa serikali na vikundi vya kiraia, Ban amesema kuna mafanikio katika kumkwamua mwanamke tangu ashike wadhifa huo mwaka 2006 lakini bado kwingineko ukatili, ukiukwaji wa haki za mwanamke vinaendelea.

Hata hivyo amesema..

(Sauti ya Ban)

“Heshima zangu kwa maelfu ya wanawake mashujaa ambao nimekutana nao wakati za ziara zangu. Napongeza pia wanaume ambao wameungana nasi kwa sababu wanafahamu kuwa haki za wanawake ni haki za binadamu ambazo tunazisaka kwa maslahi ya kila mtu.”

 Miongoni mwa washiriki wa mkutano huo utakaoendelea hadi tarehe 24 mwezi huu ni Gisele Ngungua Sangua, kutoka shirika lisilo la kiserikali la Alfa huko DR Congo yeye anazungumzia hali ya mwanamke nchini mwao.

(Sauti ya Gisele)