Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya amani ya Syria yaanza tena, bado sintofahamu ni kubwa

Mazungumzo ya amani ya Syria yaanza tena, bado sintofahamu ni kubwa

Mazungumzo ya amani ya Syria yameanza tena mjini Geneva, Uswisi hii leo, wakati vita nchini Syria vikitimu miaka mitano, na huku sitisho la mapigano likiwa limedumu kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amewaambia waandishi wa habari kwamba sasa ni wakati wa ukweli, akisikitishwa kwamba bado kuna vikwazo vingi kwa upatanishi na sintofahamu kubwa baina ya pande kinzani za mzozo.

(Sauti ya Bwana De Mistura)

“ Iwapo, wakati wa mazungumzo hayo na raundi zingine zitakazofuata, hatutaona dalili yoyote ya utashi wa kupatana, tukitumai kwamba haitatokea, basi tutapeleka suala hili mbele ya wale wanaoweza kuwa na ushawishi, yaani Urusi, Marekani na Baraza la Usalama.”  

 Mjumbe Maalum ameongeza kwamba anategemea kuongoza raundi tatu za mazungumzo mjini Geneva, huku akisistiza kwamba hakuna mpango mbadala mazungumzo endapo yakishindikana, zaidi ya vita kali kuendelea kutawala..