Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CAR kuanzisha mahakama maalum ya uhalifu : mtalaam huru

CAR kuanzisha mahakama maalum ya uhalifu : mtalaam huru

Mtalaam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Marie Thérèse Keita Bocoum amepongeza jitihada za serikali ya nchi hiyo na jamii ya kimataifa katika maandalizi ya kuanzisha mahakama maalum ya uhalifu.

Mtalaam huyo ambaye amehitimisha ziara yake ya siku kumi nchini humo baada ya awamu ya pili ya uchaguzi wa rais, amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Bangui.

(sauti ya Bi Keita Bocoum)

“Serikali ya mpito imepitisha sheria hiyo ya kihistoria ya kuanzisha mahakama hiyo ambayo itahukumu watekelezaji wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu. Ni lazima raia wa CAR waweze kuona kwamba hizo si ahadi tupu na kwamba waliotendea uhalifu wataadhibiwa.”

Bi Keita Bocoum ametoa wito pia kwa jamii ya kimataifa isaidie serikali ya CAR katika kuanzisha mahakama hiyo.