Skip to main content

Ban Ki-moon alaani shambulio la kigaidi Uturuki

Ban Ki-moon alaani shambulio la kigaidi Uturuki

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi lililotokea leo kwenye mji mkuu Ankara, nchini Uturuki, ambapo makumi ya watu wameuawa na kujeruhiwa.

Taarifa ya msemaji wake imesema kwamba Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga, huku akiongeza kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kushikamana na raia na serikali ya Uturuki wakati huu mgumu.