Skip to main content

UNWTO yalaani mashambulizi ya kigaidi Côte d'Ivoire

UNWTO yalaani mashambulizi ya kigaidi Côte d'Ivoire

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Utalii Duniani UNWTO limelaani shambulio la kigaidi lililotokea leo kwenye hoteli, mjini Grand Bassam, nchini Côte d'Ivoire, na kusababisha vifo kadhaa.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, UNWTO imetuma salamu zake za rambirambi kwa familia na rafiki za wahanga, pamoja na raia wa Côte d'Ivoire.

Katibu Mkuu wa UNWTO Taleb Rifai amenukuliwa akisema wameshtushwa wana na kitendo hicho cha ghasia ya kutisha.

Aidha UNWTO imekariri uaminifu wake kwa sekta ya utalii ya Côte d'Ivoire ambayo imeendelea kukua katika kipindi cha miaka michache iliyopita, na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo nchini humo.