Miaka mitano baada ya kuzuka vita Syria hali bado ni tete japo kuna matumaini:

Miaka mitano baada ya kuzuka vita Syria hali bado ni tete japo kuna matumaini:

Miaka mitano baada ya vita vilivyoghubikwa na ukatili na madhila mengi zaidi ya Wasyria robo milioni wamepoteza maisha, Zaidi ya nusu ya watu wote wamelazimika kukimbia makwao na wengine wapatao milioni 4.6 ni kama hawaishi katika maeneo ambayo wachache wanaweza kuishi na misaada haiwafikii.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wao, Syria leo hii ni haitamaniki na itachukua vizazi na vizazi kuijenga upya. Watu milioni 4.8 wameikimbia nchi kabisaa.

Taarifa hiyo imema hata hivyo katika wiki chache zilizopita ishara ya matumaini imeanza kuonekana , mabomu machache yamekuwa yakidondoka, fursa za kutoa misaada ya kibinadamu zimeanza kujitokeza, pande zote kinzani zimeanza kujiandaa kuketi pamoja kuzungumza, hii ni hatua ya kukaribishwa.

Umoja wa Mataifa na wadau wengine wanatumia fursa hiyo ya matumaini kuwafikia maelfu ambao wamekuwa bila msaada kwa muda mrefu. Na wamefanikiwa kuwafikia watu milioni 6 tangu mwanzoni mwa 2016.

Hata hivyo wameonya kwamba mpaka pande zote zitakapokoma kushambulia raia, shule, masoko na hospitali wataendelea kushinikiza pande hizo kuhusu wajibu wao na kuwawajibisha.

Wametoa wito kwa pande zote , wa kitaifa na kimataifa kuwa kumbukumbu hii ya miaka mitano iwe ni ya mwisho na kwa mazungumzo ya kisiasa kuleta amani ya kweli na kukomesha madhila kwa watu wa Syria.