Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ustawi wa watoto wa kike huleta manufaa kwa familia- Eliasson

Ustawi wa watoto wa kike huleta manufaa kwa familia- Eliasson

Watoto wa kike na wanawake wanapopata kipato, wanawekeza mara 90 zaidi kwenye familia zao kuliko wafanyavyo wavulana na wanaume.

Hiyo ni kauli ya Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson aliyotoa kwenye kikao cha ngazi ya juu kuhusu umuhimu wa kuwekeza kwa mtoto wa kike kama njia ya kufanikisha ajenda 2030.

Eliasson amesema kila mwaka anaoongeza mtoto wa kike masomoni, unaongeza kipato chake kwa asilimia 20 na ndivyo ustawi wake utakuwa bora sambamba na familia na jamii yake.

Hata hivyo amesema inasikitisha baadhi ya maeneo duniani mtoto wa kike inabidi awe jasiri ili kuhudhuria shule kutokana na mizozo, ubaguzi ilihali elimu ni haki yake ya msingi.

Hivyo amewaeleza washiriki wa kongamano hilo lililoandaliwa na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA kuwa..

(Sauti ya Eliasson)

“Tunafahamu fika matatizo yanayokumba wasichana barubaru ulimwenguni kote. Hebu na tushike kasi kutoka kwa wanawake na wasichana jasiri ili hatimaye tupate majawabu ya shida zao. Tukifanya hivyo, tutasongesha hoja zinazohusiana za amani, maendeleo na haki za biandamu. Wasichana wetu barurabu wataongoza mabadiliko kueleka mustakhbali mpya.”