Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu waliotawanywa na mapigano Iraq wamekwama katika kambi:UNHCR

Watu waliotawanywa na mapigano Iraq wamekwama katika kambi:UNHCR

Nchini Iraq ongezeko la watu wanaotawanywa na machafuko wamekuwa wakilazimishwa kuhamia kwenye makambi na kisha kuzuiliwa kuondoka limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumiwa Wakimbizi UNHCR.

Takribani kambi nne nchini humo zimekuwa zikitekeleza hatua hiyo ambayo UNHCR inasema haiendani na masuala halali ya usalama kama anavyofafanua msemaji wa shirika hilo Ariane Rummery..

(SAUTI YA ARIANE RUMMERY)

“Sababu inayotuongezea hofu kuhusu maendeleo ya mwenendo huu ni kwamba uhuru wa kutembea ni muhimu kwa waliotawanywa na vita, kuweza kutekeleza haki zingine, kama fursa za kufanya kazi, chakula, huduma za afya na msaada wa kisheria”

UNHCR inasema ni muhimu kwa makambi kuendeleza wajibu wao wa kibinadamu.